Saturday, August 13, 2016

KESHENI MKIOMBA

KESHENI
Basi kesheni, kwa sababu hamwijui siku wala saa. Mathayo 25:13.
Kuja kwa Kristo kutakuwa kama ambavyo ingelikuwa usiku wa manane, wakati watu wote wakiwa wamelala. Itakuwa vema kwa wote kuandaa hesabu zao kikamilifu kabla ya jua kutua. Matendo yote yapaswa kuwa sahihi, biashara zote zapaswa kuwa za haki, kati ya mtu na mwenzake. Hali zote za kutokuwa waaminifu, mazoea yote ya dhambi yapaswa kutupiliwa mbali. Mafuta ya neema yapaswa kuwa katika vyombo vyetu pamoja na taa zetu. . . Kwa hakika itakuwa huzuni kwa yule ambaye hali ya roho yake imekuwa na mfano tu wa utauwa huku akizikataa nguvu zake; ambaye amekuwa akimuita Kristo Bwana, Bwana, na bado hana mfano wake wala maandiko yake. ..
Kwa neema Mungu anatoa siku ya rehema, muda kwa ajili ya jaribio na maonjo. Anatoa mwaliko: “Mtafuteni Bwana maadam anapatikana, mwiteni maana yu karibu”. . .
Leo sauti ya rehema inaita, na Yesu anavuta watu kwa kamba za upendo; lakini siku yaja ambapo Yesu atavaa mavazi ya kisasi. . . Uovu wa dunia linaongezeka kila siku, na hatua fulani inapokuwa imefikiwa, kitabu kitakuwa kimefungwa, na hesabu zitakuwa zimekamilishwa. Hakutakuwa na kafara kwa ajili ya dhambi tena. Bwana anakuja. Kwa muda mrefu rehema imenyoosha mkono wa upendo, subira na uvumilivu, kuelekea kwa dunia yenye hatia. Mwaliko umetolewa, “Hebu na ashikilie nguvu zangu...” Lakini watu wametumia vibaya rehema na kukataa neema.
Kwa nini Bwana amekawiza ujio wake hivyo? Jeshi zima la mbinguni linasubiri kukamilisha kazi ya mwisho kwa dunia hii iliyopotea, Kazi hiyo haijakamilishwa kwa sababu wachache wanaodai kuwa na mafuta ya neema katika vyombo vyao na taa zao, hawajakuwa nuru ing’aayo na kuiangaza dunia. Ni kwa sababu wamishenari ni wachache. . .
Kila juma linapopita linamaanisha juma moja limepungua, kila siku ipitayo inaashiria siku moja ya karibu zaidi kufikia wakati uliowekwa kwa ajili ya hukumu. Inasikitisha kwamba wengi wanayo dini ya msimu - dini inayotegemea hisia na kutawaliwa na misisimko. “Yeye atakayevumilia hadi mwisho ndiye atakayeokoka.” Hivyo jichunguzeni na kuhakikisha kama mnayo mafuta ya neema ndani ya mioyo yenu. Kuwa na mafuta haya kutatengeneza ule utofauti utakaohitajika katika hukumu.

MAKAMU WA RAIS

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewahimiza wananchi wa Tanzania Bara na Zanzibar kuunga mkono jitihada zinazofanywa na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika mapambano dhidi ya rushwa,ufisadi kama hatua ya kukomesha tabia hiyo ambayo inarudisha nyuma maendeleo ya wananchi.
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo 13-Aug-16 wakati anahitimisha kilele cha sikukuuu ya Wakizimkazi katika kijiji cha Kizimkazi Mkunguni wilayani ya Kusini Unguja – Zanzibar ambaye yeye ni mwasisi wa sikukuu hiyo ambayo inatumiwa na wakazi wa maeneo hayo kufanya michezo mbalimbali ya jadi pamoja na kujadili na kuweka mipango na mikakati ya kujiletea maendeleo kwa ushirikiano na viongozi wao.
Makamu wa Rais amewahakikishia kuwa serikali itaendelea kuchukua hatua kali kwa watendaji wanaorudisha nyuma maendeleo ya wananchi ikiwemo ubadhirifu wa fedha za umma ili kukomesha tabia hiyo.
Amesema kuwa ili wananchi waweze kupata maendeleo ya haraka ni muhimu wananchi wakaimarisha ushirikiano miongoni mwao katika kubaini changamoto zinazowakabili na kushirikiane na viongozi wao katika kuzitafutia ufumbuzi changamoto hizo.
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema yeye kama kiongozi wa kwanza kupata wadhifa huo kutoka kwenye kijiji cha Kizimkazi- Zanzibar ataendelea kushirikiana wananchi hao kutatua matatizo yanayowakabili wananchi hao ikiwemo tatizo la upatikanaji wa maji.
Makamu wa Rais pia amehimiza wananchi wa Kizimkazi kutafuta eneo haraka kwa ajili ya ujenzi wa shule ya awali ambayo bado ni tatizo kubwa katika eneo hilo ili aweza kuwasaidia katika ujenzi wake kama hatua ya kuondoa kero ya watoto kushindwa kupata elimu ya awali.
Katika Risala maalum ya wananchi wa kijiji cha Kizimkazi na Katibu wa Sherehe hizo Said Ramadhani Mgeni kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan wamewapongeza viongozi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa jitihada wanazofanya za ukusanyaji wa mapato ya serikali na wamesema wanaimani kubwa kuwa fedha zinazopatikana zitatumika katika kuinua uchumi na kujenga ustawi wa Jamii bora wananchi.
Wananchi hao wameahidi kuwa watadumisha na kuimarisha ushirikiano kati yao na serikali hasa katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Baadhi ya Viongozi wa wilaya na Mkoa wa Kusini Unguja waliopata nafasi ya kuzungumza katika hafla hiyo ya hutimisha sikukuu ya wakizimkazi wamewaomba wananchi kudumisha amani na utulivu katika maeneo yao.
Imetolewa na
Ofisi ya Makamu wa Rais
13-Aug-16.